Mke wa Marehemu Prof. Jwani Mwaikusa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mume wake kipenzi nyumbani kwake eneo la Mkonde, Kunduchi Salasala leo kabla ya mazishi yaliyofanyika leo marehemu Mwaikusa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na mwanasheria, Mwaikusa atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika masuala mazima ya sheria nchini lakini pia wanafunzi aliowaachia ujuzi katika chuo kikuu cha Dar es salaam watamkumbuka sana Mungu, aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Prof. Jwani Mwaikusa Amin.
Umati wa watu waliojitekeza nyumbani kwa marehemu Prof. Jwani Mwaikusa yaliyofanyika nyumbani kwae Kunduchi Salasala leo marehemu aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake juzi.
Mwili wa marehemu Profesa Mwaikusa ukishushwa ndani ya kaburi kwa mashine maalum.
Mke wa Marehemu Profesa Mwaikusa akiweka shada la Maua kwenye kaburi la marehemu mume wake katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Mkonde, Kunduchi Salasala .leo picha kwa hisani ya www. mohammeddewaji.blog.




1 comments:
inasikititisha kwani hao majambazi hayajapatikana ni nilisoma kwenye gazeti la majira wanasema pia waliiba vocher na pesa dukani jirani na kwa prof je hizo kadi hazina serial number? kama dukani wanarecord za serial number kuna huwezekano wowote wakufuatilia hizo kadi nani kazitumia maana simu za siku hizi zimesajiliwa ni mimi mdau wa texas
Post a Comment