Rais Kikwete apokea 10/m kutoka TAG kwaajili ya Mashuka hospitali ya Dodoma na kufungua Mkutano Mkuu wa TAG!

Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Dr.Barnabas Mtokambali akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni kumi(10m/) kama mchango wa kanisa hilo kwa ajili ya kununulia mashuka ya wagonjwa kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano Mkuu wa Kanisa hilo uliofanyika chuo Kikuu Dodoma ambapo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi.Rais Kikwete alikabidhi mchango huo kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhandisi Dr.James Nsekela.
(Picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshika bendera ya taifa pamoja na Maaskofu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God wakati wa sala maalumu ya kuiombea amani na ustawi Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa kanisa hilo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana.Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God katika ukumbi wa Chimwaga chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana(picha na Freddy Maro)

Baadhi ya viongozi waandamizi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God wakionyoosha mikono wakati was ala maalumu ya kuiombea amani na ustawi Tanzania wakati wa mkutano mkuu wa kanisa hilo uliofanyika katika chuo kikuu cha Dodoma leo mchana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment