Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi visiwani Zanzibar, Dk Shein, asubuhi ya leo amepokelewa kwa kishindo mjini Zanzibar, wakati akiwasili kutoka jijini Dare s Salaam, akiwa sambamba na mgombea mwenza, Dk Mohammed Ghalib Bilal. Dk Shein akiwa na msafara wake, waliwasili katika bandari ya Zanziabar, wakitumia boti ya Kilimanjaro II, na kulakiwa na mamia ya wananchi, viongozi wa kitaifa na viongozi wa chama. Hii ni mara ya kwanza kwa Shein kutua Zenji tangu alipotangazwa kuwania Urais wa Zanzibar hivikaribuni mjini Dodoma. Baada ya mapokezi hayo, msafara ulielekea kwenye Ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, ambako baada ya kusaini kitabu cha wageni, alikutana katika mkutano wa siri na wazee wa Zanzibar. Picha kwa hisani ya (www.globapublisherstz.com)
DR. ALI MOHAMED SHEIN ALIPOTUA ZANZIBAR LEO!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







0 comments:
Post a Comment