KATIBU MKUU MWAKALEBELA ANG'ATUKA TFF!

Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF FREDRICK MWAKELEBELA kushoto hataki tena kuendelea na kazi TFF kwani ameamua kuingia kwenye siasa rasmi , Amesema hayo wakati akitangaza rasmi kuondoka katika shirikisho hilo na kuingia kwenye siasa.

MWAKALEBELA mesema kama kamati ya utendaji ilikuwa inamtaka tena kuendelea na kazi hiyo, ijaribu kutafuta mtu mwingine lakini si yeye tena kwani ameamua kung'atuka katika wadhifa huo na kwenda kuwatumikia wananchi wa jimbo la Iringa Mjini.


Amesema kwa sasa anaelekeza nguvu zake katika jimbo la IRINGA MJINI .
na natarajia kukabidhi ofisi mara baada ya kamati ya utendaji ya TFF kukaa Julai 17 mwaka huu.

Pia ametoa shukurani zake za dhati kwa watu wote walioshirikiana naye katika kuendeleza soka hapa nchini. Picha kwa hisani ya GPL.

Add Image

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment