Rais Kikwete akutana na mtoto mlemavu Frank Charles ikulu ya mjini Dodoma, apokelewa kwa shangwe Dar es Salaam!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete(kushoto) wakiwa na mtoto Frank Charles Valia (9) ikulu ya mjini Dodoma leo asubuhi.Mtoto huyo Frank(watatu kushoto) na baba yake mlezi Khamis Said(wapili kushoto) walikwenda ikulu ya Dodoma kumshukuru Rais Jakaya Kikwete aliyegharamia matibabu ya Fank huko India ambapo anatarajiwa kurudi kwa matibabu zaidi baada ya miezi sita.Mtoto Frank alipata ulemavu wa kupinda mgongo baada ya kuanguka kutoka juu ya mti.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mara tu alipowalisili akitokea mjini Dodoma ambapo alilihutubia Bunge(picha na Freddy Maro)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment