Kutoka kushoto ni Meneja wa kampuni ya Macro software System Bw.Ibrahim Goebles akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam akiwa na msemaji wake mkuu Bw. Sebastian Ndege.(kulia)
Meneja mkuu wa biashara wa kampuni ya Macro software Systems (Macrosoft) Bw.Ibrahim Goebles ametangaza nia ya kugombea kiti cha udiwani katika kata ya Kivukoni Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Bw.Ibrahim amesema matatizo waliyonayo wananchi wa kata ya Kivukoni ni machache kama vile Ulinzi,Usafi na Utumiaji mzuri wa rasilimali zilizopo katika kata hiyo,na kwa kuwa alioombwa na walio wengi na kuzungumza na wana Kivukoni Vijana na wazeeameamua kutangaza nia ya kugombea udiwani akiwa na ari na kiu ya kuleta maendeleo katika kata hiyo.
Aidha Bw.Ibrahim amesema sababu za kugombea ni kuwajibika kama raia katika kutoa mchango wake wa jumla na kuongeza safu ya vijana katika kuleta maendeleo,kuleta fursa sawa,bunifu na mpya za maendeleo kupitia uwakilishi wa vijana katika ngazi ya udiwani kata hiyo pamoja na kuwa kiuongo na kiunganishi muhimu cha maendeleo ya wakazi Kivukoni katika sekta zote muhimu.
Akihitimisha Bw.Ibrahim amesema ana nia ya kweli ari mpya na kasi yenye kuleta maendeleo inayohitaji wana kivukoni wenyewe kwa kuona changamoto na fursa zilizopo ndani ya kata ya Kivukoni hazitambuliki kwa miaka mingi anaomba kwa ridhaa yake kuwa Diwani wa kata hiyo ili kutumia kipaji, uwezo na elimu kuleta maendeleo na mabadiliko yenye maridhiano na hali halisi ya Kivukoni.
hisani ya www.mohammeddewaji.blog






0 comments:
Post a Comment