Wateja wa Vodacom wanaotumia huduma za intaneti zinazotolewa na Vodacom Tanzania wataendelea kupata huduma hiyo hata kama matatizo ya mkongo wa mawasiliano yanayotokea mara kwa mara hapa nchini yataendelea.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba alisema kwamba hayo yote yamewezekana kutokana na uwekezaji mkubwa ulifanywa na Vodacom katika huduma hiyo.
“Mtandao wa Vodacom Tanzania utaendelea kuwa hewani na kuwaunganisha wateja wake na tovuti mbalimbali Duniani hata kama mkongo wa mawasiliano wa baharini utapata hitilafu”
Mkongo huo unasambaza huduma za mawasiliano ya intaneti kwa nchi za Uarabuni, Ulaya na Ukanda wa Afrika Mashariki,”
Hivi karibuni mkongo huo umekuwa ukikumbwa na hitilafu ambazo zimekuwa zikiwakosesha wateja wengi huduma na mara ya mwisho hitilafu ilitokea Mombasa nchini Kenya mwanzoni mwa mwezi huu.
“Kutokana na uuwekezaji wetu katika huduma hiyo sanjari na ubora wa mtandao wetu, wateja wetu wameendelea kuunganishwa hata kama mkongo wa mawasiliano ulipata mushkeli” alisema na kuongeza “Upatikanaji wa mtandao wa intaneti kwa uhakika ni jambo muhimu sana, ndiyo maana uwekezaji wetu katika intaneti ni wa uhakika,” alisema.
Alisema ili kukidhi haja ya mahitaji mbalimbali ya wateja wake Vodacom inatoa huduma za intaneti kwa bei nafuu na rahisi ambayo kila Mtanzania anaweza kuimudu.
Wateja wa Vodacom Tanzania wanapata huduma kwa bei nafuu kwa mfano, kwa mteja ananunua MB kwa shilingi 120 pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT), ambayo ni sawa na tozo la shilingi 0.12 kwa kila KB.
Kutokana na bei ndogo ya kila MB mteja anaweza kununua kifurushi cha MB ambacho kitakidhi mahitaji yake.
Anasema kwa sasa Vodacom imekuja na huduma mpya ya Cheka Intaneti ambayo ambayo ina mwezesha mteja wa Vodacom kutumia huduma ya Intaneti Kwa wale watumiaji wa simu za mikononi kwa shilingi 500.
Watumiaji wa kompyuta wao wanaweza kupata huduma ya intaneti ya Vodacom kwa shilingi 10,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na MB 250. Viwango vingine vya vifurushi ni pamoja na MB 500 kwa Sh. 20,000, GB 1 kwa Sh. 40,000, GB 2 kwa Sh. 70,000, GB 3 kwa Sh. 90,000, GB 5 kwa Sh. 140,000.
Alisema watumiaji wenye ofisi ndogo wanaweza kutumia GB 10 kwa Sh 270,000 na GB 20 Sh. 450,000 ambayo inaweza ikatumiwa na na mpaka watumiaji wanane.
Mwamvita alisema wateja wa intaneti wa Vodacom wenye kompyuta, Vodacom inawapa USB modem inayofaa kutumiwa na kompyuta aina ya Mac kwa Sh. 75,000 sanjari na MB 500 bure Modem hii yenye kasi inapatikana katika maduka yote ya Vodashop.





0 comments:
Post a Comment