RAIS JAKAYA ATEUA NAIBU MAKATIBU WAKUU 9!!




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameteua Naibu Makatibu Wakuu tisa (9) wa Wizara mbalimbali.


Taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 20 Julai, 2010 Jijini Dares Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon Luhanjoinaonyesha kuwa uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu hao unaanziatarehe 15 Julai, 2010 na wataapishwa rasmi siku ya Alhamisi tarehe29 Julai, 2010 saa 4.00 asubuhi.


Taarifa hiyo imewataja walioteuliwa kuwa ni pamoja na BwanaNgosi C.X. Mwihava, Kamishna Msaidizi (Nishati Mbadala) katikaWizara ya Nishati na Madini kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais.Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Bwana Luhanjo, Rais Kikweteamewateua Balozi Herbert E. Mrango ambaye ni Mkurugenzi waIdara ya Ushirikiano wa Kanda katika Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara yaMiundombinu; Balozi Rajab Gamaha ambaye ni Balozi wa Tanzanianchini Uganda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Kimataifa, na Bwana Mbogo Futakamba,Mkurugenzi wa Umwagiliaji na Ufundi ambaye sasa anakuwa NaibuKatibu Mkuu katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji.


Katika Uteuzi huo, Rais Kikwete pia amewateua Dk. YohanaL. Budeba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti waUvuvi (TAFIRI) kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo yaMifugo na Uvuvi, na Bibi Maria H. Bilia ambaye ni Katibu Tawala waMkoa wa Kagera kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


Aidha, Rais Kikwete amewateua Bibi Nuru H.M. Mlao ambayekwa sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha kuwa Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii; Bwana Hussein A. Katanga ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro kuwa Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, na BwanaJob D.Masima ambaye ni Mkurugenzi katika Wizara ya Ushirikianowa Afrika Mashariki kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa.Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment