MFANYAKAZI WA TSN ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA VITI MAALUM ULEMAVU (UWT)

MFANYAKAZI wa Shirika la Magazeti ya Serikali(TSN), Zaituni , ambaye ni mlemavu wa miguu jana alitangaza nia yake ya

kugombea ubunge wa viti maalum
kundi la walemavu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
mwandishi wa habari wa kujitegemea katika gazeti la Gurdian, Mwananchi na Express. kabla ya kuajiriwa na TSN kama mwandishi wa habari
alitangaza nia hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,ambapo alisema amekuwa ni mwanaharakati wa kupigia nia haki za watu wenye ulemavu tangu akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi .

Saeedia ambaye pia aliwahi kuwa
Akizungumzia kuhusu lengo lake ya kugombania nafasi hiyo alisema ni kuiwakilisha jamii ya watu wenye ulemavu katika Bunge la Jamhuri Muungano Tanzania. “Nitasimamia katika sheria ya walemavu ya kimataifa kwa kuwaelimisha walemavu wenzangu na jamii kwa ujumla kuhakikisha jamii inaacha fikra potofu kwamba upungufu wa viungo mwilini hakuzii kushiriki au kushirikishwa kwenye shughuli za uzalishaji mali na maendeleo iwe nchini au ulimwenguni,” alisema Zaituni.
Aliongeza pia akichaguliwa atatilia mkazo kupata orodha ya watu wenye ulemavu na kazi wanazozifanya ili kuwatambua, kuhakikisha sera na sheria zinazotungwa zinazingatia haki na maslahi ya walemavu, kusimamia ipasavyo utekelezaji wa sera na sheria ya watu wenye ulemavu na kuhamasisha makundi yote ya jamii, kutambua kuheshimu na kuzingatia haki na mahitaji ya walemavu .


Saeedia ambaye ana elimu ya Stashahada ya Ukutubi, Udokometa na Uhifadhi Nyaraka na Kumbukumbu, kutoka Chuo Cha Ukutubi na Uhifadhi wa Nyaraka Tanzania(SLADS) jana alichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi ya UWT mkoa wa Dar es Salaam.Hivi sasa ni mwanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini katika fani ya Mawasiliano ya Umma.


Pia ni mchora katuni maarufu wa kujitegemea na vielelezo mbalimbali katika magazeti, majarida, mabango na hata vitabu mfano katuni ya kichen party kwenye gazeti la Sunday News (mwaka 2000- 2006), Vijarida vya Haki Elimu, Care international Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment