MATUKIO YA MKUTANO WA KAMATI KUU NA USHINDI WA DR.ALI MOHAMED SHEIN!!

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akiwashukuru wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kwa kumchagua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM. (Picha na Ferdy Maro).

Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo Dr.Ali Mohamed Shein aliibuka mshindi katika ugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM jana usiku mjini Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalumu cha Halmshauri kuu ya CCM mjini Dodoma jana usiku.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa White house mjini Dodoma jana usiku.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya ushindi wa Dr.Ali Mohamed Shein kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM jana usiku.
Baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM wakiwa katika kikao maalum kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi jana usiku mjini Dodoma.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment