GENEVIVA NDIYE REDDS MISS TEMEKE 2010!!

Vodacom Miss Temeke 2010 Geneviva Emmanuel akipungia mashabiki mkono mara baada ya kumtangaza mshindi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam kushoto ni mshindi wa pili Anna Daud na kulia ni mshindi wa tatu Britania Urasa,

Mwenyekiti wa kamati ya Miss Temeke Bw. Benny Kisaka alisikika akisema hizi ndiyo pini za Miss Temeke zitakazo wakilisha shindano la taifa la Vodacom Miss Tanzania hapo baadae na tuna uhakika na pini hizi kwamba zitatikisa katika shindano hilo kubwa nchini na kushinda hatimaye kumpata Miss Tanzania kutoka kandaTemeke.

Hii ndiyo tano bora ya Miss Temeke 2010 mara baada ya majaji kutangaza matokeo hayo.
Viongozi wa kamati ya Miss Tanzania ambao ndiyo walikuwa majaji wakikuna vichwa ili kupata mshindi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa TCC Sigara Chang'ombe usiku wa kuamkia leo kutoka kulia ni Mkurugenzi Hashim Lundenga, Mwenyekiti Prashant Patel na Katibu Mkuu Bosco Majaliwa.
Hatimaye baba na mwana walipanda jukwaani pamoja wakiimba wimbo wa "Zela" kushoto ni mzee Zahir Ally Zorro baba yake Banana na kulia ni mwanae Banana Zorro wakiimba jukwaani.
Baada ya warembo kupita jukwaani na vazi la jioni ukwadia wakati wa kupata warembo watano bora ndipo mwanamuziki Banana Zorro na kundio lake la B.Band likapanda jukwaani ili kutoa burudani kama unavyowaona kulia ni Banana Zorro na kushoto ni Siza Azizi waiimba kwa hisia.


Wakaanza kupita jukwaani na vazi la jioni.
Pozi tofauti za vazi la ufukweni.
Baada ya shoo ya ufunguzi warembo walipita jukwaani na vazi la ufukweni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment