MWANAMUZIKI anayetamba kwa sasa anga ya Afrika Mashariki Kidumu anayetamba na kibao cha “Haturudi Nyuma” anatalajia kukonga nyoyo wakaazi wa Zanzibar na wageni mbalimbali kwa burudani kali ndani ya Ngome Kongwe kwenye tamasha la ZIFF 2010 kesho.
Akiongea leo Afisa wa Habari wa ZIFF 2010, Asmah Makau alisema Kidumu anatarajia kuburudisha kwenye tamasha hilo kubwa la kila mwaka ambapo ataburudisha nyimbo zake zote. “Kidumu anatarajia kuburudisha nyimbo zake zote maalufu hivyo mashabiki wasubiri burudani ambayo ataitoa live’. Alisema Asmah.
Kidumu ambaye jina lake halisi Jean Pierre Nimbona ameweza kujipatia heshima kwa kibao chake hicho cha Haturudi Nyuma alichomshirikisha Juliana Kinyomozi pia anatamba na albamu yake iliyo na nyimbo kama Umenikosea, ambazo zote zipo ndani ya albamu yake ya “Best of Kidumu Haturudi Nyuma”.
Zanzibar International Films Festival maalufu kama ZIFF 2010 mwaka huu imeingia mwaka wa 13 na imekua ya kipekee kwa wageni mbalimbali na wakaazi wa Zanzibar ambapo wanapata kuangalia filamu zaidi ya 100 na kupata burudani kutoka kwa wasanii maarufu ndani na nje ya Nchi.
Wasanii ambao mpaka sasa wamesha tumbuiza ni pamoja na Ambwene Yesaya AY, Dully Sykes, Baby J,Spec Boogie kutoka marekani,Sultan King kutoka Zanzibar huku vikundi vingine ni; B 6 Street Boys “THT wa Zanzibar’ na wengine wengi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ZIFF 2010 Martin Mhando aliwaomba wakazi kujitokeza kwa wingi ilikushuhudia filamu hizo na kujifunza. “Nyote mnakaribishwa mwaka huu wakaazi wa zanzibar kiingilio bure hivyo wanakaribishwa” alisema Mhando. Viingilo kwa wananchi ambao si wakaazi ni 10,000/= ambapo wataona filamu na kisha kuburudika na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali maalufu baaada ya kumalizika kwa filamu. Wadhamini wakuu ni pamoja na; VodaCom Tanzania, Coca-Cola, ,Grand Malt,Saadan Park, Azam Marine na wengineo.






0 comments:
Post a Comment