Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya wajasiriamali kwenye kongamano la Wajasiriamali linalozungumzia mambo mbalimbali ya wajasiriamali katika kuchangia maendeleo ya nchi, lakini pia wajasiriamali hao. kubadilishana mawazo na uzoefu katika biashara zao ili kuifikisha mbali zaidi sekta ya kiuchumi, kupitia wajasiriamali na kuwaletea maendeleo.
Kongamano hilo linakwenda pamoja na maadhimisha ya siku ya wajasiriamali na maonyesho ya taasisi mbalimbai za kibiashara na yafanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, katika picha katikati ni Bw. Paul Mashauri Mratibu wa maonyesho hayo na kulia ni Juliet Mwinuka Meneja Mradi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo mara baada ya kuzindua maonyesho hayo kweny viwanja vya Karimjee.





0 comments:
Post a Comment