JINAMIZI LA BONGO DANSI ! la "Ngoma Africa Band" lawanasa Wazungu! Ulaya.


Katika hali ya utata washabiki wa mziki huko ughaibuni wamejikuta wamenaswa na ugonjwa wakupenda "Bongo Dansi" la bendi maarufu ya mUziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Bendi"ambayo pia ina majina mengi ya utani kama vile FFU,pia "Wazee wa Kukaanga Mbuyu",Mzimu wamuziki n.k.

Bendi hiyo inayoongozwa na mwanaziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja,yenye maskani yake nchini Ujerumani,imejikuta ikiwanasa washabiki katika kila pembe za ughaibuni kutokana na mdundo wake.

Mdundo ambao unafananishwa na "JINAMIZI" kubwa lililowanasa washabiki!Kwani washabiki bila kusikia mdundo wa "Ngoma Africa Band" almaarufu FFU,bado tamasha halijakamilika!na kwa washabiki bado hakijaeleweka hadi pale watakapo sikia mdundo wa "Ngoma Africa" unarindima na washabiki kujimwaga uwanjani.

Mara nyingi Jinamizi hilo la "Bongo Dansi" huwa linafaninishwa na Pepo mwenye nguvu zaidi! na kasi kubwa!Pia Jinamizi hilo limekuwa tishio mpaka kwa maporomota wa mziki ! kwani poromota asipo weka jina la"Ngoma Africa Band" katika orodha ya bendi zitakazo tumbuiza basi mashaka ya mshike mshike wa washabiki yatalipuka kwa fujo nzito.

Jinamizi hilo la "Bongo Dansi" sio tishio tu kwa maporomota bali linawapereka puta hadi wanamziki wenyewe wa Ngoma Africa Band,hususan kiongozi wao ambaye pia ni mwimbaji Ras makunja aka kamanda wa FFU ambaye amehakikisha kuwa kila mipango yake inayofanyika lazima ifanyika kwa umakini ili kukidhi matakwa ya washabiki wa bendi hiyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment