DR. MOHAMED GHALIB BILAL NDIYE MGOMBEA MWENZA WA CCM!!

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kulia akimpongeza Dr Ghalib Bilal wakati wa mkutano mkuu wa CCM Mjini Dodoma katikati ni Waziri Mkuu Mstaafu Fredirick Sumaye.


Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia chama cha Mapinduzi CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Ghalib Bilal kutoka Zanzibar kuwa mgombea mwenza kupitia CCM kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi ujao utakaofanyika Oktoba mwaka huu na kufanya ukumbi wa Chimwaga kulipuka kwa shangwe.

Dr. Bilal alikuwa mmoja wa wanaccm walioomba kugombea urais wa Zanzibar lakini alishindwa katika kinyang'anyiro hicho baada ya makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein kuibuka mshindi kwa kura nyingi katika uchaguzi huo wa CCM, hata hivyo kwa nafasi aliyopewa Dr. Bilal ni wazi kwamba wanaccm Zanzibar Tanzania Bara watakuwa pamoja na kuifikisha Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ujumla katika kiwango cha juu katika Demokrasia, utawala bora na haki kwani kila umoja wao katika tukio hili umeonyesha ukomavu wa siasa za CCM.

Wana FULLSHANGWE tunawapongeza wanaCCM kwa hatua hiyo laikini pia tunampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tunawapongeza pia Dr. Ali Mohamed Shein kwa kuteuliwa kugombea urais wa Zanzibar na Dr. Ghalib Bilal kuwa mgombea Mwenza wa Rais Jakaya Kikwete katika Jamhuri ya Muunganoi wa Tanzania tunawakia kila mafanikio katika jukumu hili kubwa walilopewa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment