CLOUDS TELEVISHENI NA MAPINDUZI YA KWELI KATIKA BURUDANI!!

Hii ndiyo nembo ya kituo cha Televisheni cha Clouds TV iliyozinduliwa juzi kwenye klabu ya Billicanas ambayo itakuwa ikitumiwa na kituo hicho kipya na kinachotarajiwa kuleta mapinduzi ya kweli katika burudani kama ilivyo ada ya kampuni hiyo inayoogoza kwa masuala ya burudani nchini hongereni wana Clouds lakini pongezi pekee zimwendee Mkurugenzi Joseph kusaga kwa kuacha milango wazi kwa wadau wenye mawazo mazuri katika maendeleo ya burudani lakini pia kwa kuyafanyia kazi mawazo ambayo anadhani ni ya muhimu kwa maendeleo ya burudani nchini.
Mkurugezni wa Clouds Entertainment Joseph Kusaga akiongea mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa nembo itakaotumiwa na kituo cha Televisheni cha Clouds Tv iliyozinduliwa juzi kwenye klabu ya Billicanas na kuhudhuriwa na watu mbalimbali pamoja na wadau wa burudani.
Hawa ndiyo wabunifu wa mambo mbalimbali katika kituoa hicho kipya cha televisheni wakiongozwa na Mkurugenzi wa utafiti Ruge Mutahaba aliyesimama kulia mbele.
Hawa ni baadhi ya watangzania wa Clouds Tv hapa wakitambulishwa rasmi kwa wageni waalikwa.
Katikati ni mtangazaji wa Clouds Tv Zamaradi akiwa katika picga ya pamoja na Jaquline Wolper kushoto ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka.
Wanyange wa watakaoshiriki shindano la Miss Temeke Julai 9 kwenye ukumbi wa TCC Sigara Chang'ombe pia walikuwepo katika uzinduzi huo.
Kajala katikati akiwa na marafiki zake wakati wa uzinduzi wa nembo ya Clouds Tv uliofanyika kweye klabu ya Billicanas juzi usiku.
Kazi ikiendelea wakati wa uzinduzi wa nembo hiyo.
Wapiga picha wa Clouds Tv wakiwa kazini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment