MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA SABASABA JANA!!

Watanagazaji wa Shirika la Utanganzaji la Taifa TBC Miriam Migomba wa TBC FM kulia na Rehema Nangu pia TBC FM wakiwa kazini katika chumba cha habari kilichopo kwenye maonyesho hayo ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakituma salaam kwa ndugu zao na kupata maelezo mbalimbali kuhusu utendaji wa shirika hilo katika masuala ya upashaji habari hapa nchini shirika hilo nalo linashiriki katika maonyesho ya 34 biashara ya kiamtaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.

Msemaji mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ingiahedi Mduma aliyekaa katikati mstari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzie katika banda la wizara hiyo kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa hii ilikuwa jana.
Wadau kutoka Wizara ya Uchumi na Fedha ni full kulipuka tu kama unavyowaona katika picha hizi.
Dada Roida Afisa habari wa shiriki la viwango nchini TBS kushoto pamoja na mwenzake Mary Meela afisa viwango TBS wakitoa maelekezo kwa mmoja wa watu waliowatembelea katika banda lao kwenye viwanja vya sabasaba jana.

Wadau kutoka msajili wa makampuni Brela nao wapo katika maonyesho ya 34 ya biashara ya kimataifa yanaoendelea sasa kwenye viwanja vya sabasaba kulia ni mdau Noel Shani na wenzake.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment