UZINDUZI WA MKAKATI WA UHIFADHI BAHARI, MAFIA.

Mhifadhi mfawidhi wa Hifadhi ya Bahari Mafia Bw. George Msumi akitoa ufafanuzi kwa Katibu mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Christopher Sayi (katikati) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Ruth Mollel (kulia) kuhusu nyavu za kuvulia samaki zisizokidhi viwango zilizokamatwa kutoka kwa wavuvi haramu katika ukanda wa Pwani wa bahari ya Hindi leo wilayani Mafia wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Hatua za Haraka za kuhifadhi Mazingira ya Bahari, ukanda wa Pwani, Maziwa, mito na Mabwawa Picha na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Katibu mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Christopher Sayi akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Mafia Manzie Omari Mangochie vitabu vyenye mwongozo wa Mkakati wa Hatua za Haraka za kuhifadhi Mazingira ya Bahari ukanda wa Pwani, Maziwa, Mito na Mabwawa leo wilayani Mafia.

Sehemu ya eneo la Bahari ya Hindi iliyotunzwa na kuhifadhiwa vizuri katika Hifadhi ya Bahari Mafia.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment