Waziri wa mambo ya nje wa Algeria anaesheghulia ushirikiano wa masuala ya Afrika Mhe. Abdelkader Messah (kushoto) na kulia ni Mhe. Benard Membe wakibadilishana hati za Ushirikiano kwenye Hotel ya Movenpick jijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Anna Itenda -Maelezo)
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI ya Algeria imeahidi kuisaidia Tanzania kuondoa msongamano wa magari katika miji mikubwa hasa Dar es Salaam, kwa kuboresha miundombinu ya reli ya barabara za kisasa.
Hayo ya yamesemwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutia saini Mkataba wa Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na Waziri wa Algeria anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Afrika, Abdelkader Messahel jijni Dar es Salaam kwenye hoteli Movein Peak.
Utiaji saini huo umefanyika wakati wa mkutano wa nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kudumu(JPC) uliohusisha nchi hizo na kuongozwa na Waziri Membe, akiwemo Waziri Messahel, ulioanza Julai 18 mwaka huu na kumalizika leo Julai 20, mwaka huu (jana).
“Algeria ni wataalamu wa ujengaji wa barabara za flyovers, reli za chini, umeme,hivyo tutasaidiana kutatua tatizo la foleni kutokana na msongamano wa magari kwa kujenga barabara hizo na za kisasa katika jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, ikiwemo kuboresha miundombinu ya reli ambayo itakuwa inasafisha watu kutoka pembezoni mwa jiji kuja mjini,” alisema Waziri Membe huku akiongeza kuwa atahakikisha yote yaliyozungumza na kukubaliana yanatekelezwa.
Waziri Membe aliyataja maeneo mengine ya ushirikiano huo kuwa ni kilimo, elimu, afya ,mabadilishano ya kibiashara,Utalii, Teknolojia ya Mawasiliano na Habari, Nyaraka za Taifa. Mengine ni ulinzi na usalama na nishati na madini, ambapo kampuni ya Algeria(SONATRACH) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) zimekubali kupeana taarifa kuhusu masuala ya mafuta na kufanya tafiti.
“Kusainiwa kwa mkataba huu ni hatua moja muhimu kati ya Tanzania na Algeria katika mkakati wa ushirikiano wa kiuchumi,” alisisitiza. Naye Waziri wa huyo wa Algeria , Messahel alisema mkataba huo uliotiwa saini ni wa kipindi cha miaka miwili (2010 hadi 2012) ,hivyo utaimarisha ushirikiano zaidi kati ya Tanzania na Algeria . Aliongeza kuwa anamshukuru Rais Jakaya Kiwete kwa ushauri wake alioutoa wakati wa mazungumzo yake ukiwemo ujumbe ulioongozana naye, pia aliwashukuru wataalaumu mbalimbali.
ALGERIA NA TZ KUTATUA TATIZO LA MSONGANO WA MAGARI!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment