KUBADILISHA MFUMO WA GARI LAKO ILI KUTUMIA GESI NI BEI NAFUU TU!!

Mratibu wa UDBS Alumni Association Bw. Deogratias Mboma akizungumza nma waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotangaza kuhusu taasisi hiyo kuanza kazi ya kubadilisha mfumo wa magari ya petroli kutumia gesi asilia,
Amesema utaratibu huo ni mzuri na unaunguza gharama kwa kiasi kikubwa sana huku ukiambatana na kulinda uchafuzi na uharibifu wa Mazingira, a,mesema kwamba kwa magari madogo ya petroli ili kubadilisha mfumo huo inagharimu kiasi cha shilingi milioni moja na laki tatu mpaka milioni moja na laki sana kutegemeana na ukubwa wa tank la mafuta.
Wanaofuatia katika picha ni Eng Joyce Kisamo wa shirika lka maendeleo ya Petroli TPDC na mwisho ni Andrew Kitomari mshauri kutoka Benki ya Biashara NBC.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment