Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe akiongea na waandishi wa hyabari leo kwenye ukumbu wa mkutano wa wizara hiyo wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mkutano wa nchi za Kiafrika na Ufaransa uliofanyika hivi karibuni Copenhagen Denmark na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo migogoro ya kudumu nchini Somalia na nchi nyingine kadhaa katika bara la Afrika.
Waziri Membe amesema jambo lingime kubwa lililozungumzwa ni ni kuhusu bara la affrika kupata viti viwili vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kura ya Turufu kwani matatizo mengi ya kiusalama ambayo yamekuwa yakijadiliwa kwenye baraza hilo yanahusu Afrika hivyo ni muhimu afrika ikapata uwakilishi wa kudumu na kura ya turufu katika baraza hilo la usalama ili ipate nafasi ya kuchangia hoja zake kwa uwakilishi ulio na nafasi zaidi.
Kuhusu Somalia amesema Tanzania kama ilivyoahidi mwanzo iko tayari kutoa mafunzo ya kijeshi na Polisi kwa askari wapatao 1000 kutoka Somalia katika kushiriki kuleta amani Somalia
0 comments:
Post a Comment