MAKHIRIKHIRI KUTUMBUIZA KESHO JUNI 4 DIAMOND JUBILEE!!

Kiongozi wa kundi la Makhirikhiri Mosses Malapela alipotua na kundi lake hapa nchini hivi karibuni kulia ni mmoja wa waratibu wa ziara hiyo hapa nchini kutoka Times Radio Scolastica Mazula.

MKURUGENZI wa Maedeleo ya Utamaduni Wizara Habari Utamaduni na Michezo,Profesa Hermas Mwansoko leo anatalajiwa kuwa geni rasmi katika oonyesho la kundi la Makhirikiri ukumbi wa Diamond Jubilee.

Kwa mujibu wa mratibu wa ziara ya kundi hilo, Scholastica Mazula, alisema kuwa Profesa mwansoko atakuwa mgeni rasmi ambapo aliwataka wapenzi kujitokeza kwa wingi katika onyesho hilo litakalokuwa la kukata na shoka.

“Tunaomba wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho hilo, kwani watafurahia shoo ya kundi hilo pamoja na wasanii mbalimbali wa hapa nchini ambao watawasindikiza, wakiwemo Wanne Star,Chege, na wengine wengi, huku shoo hiyo ikitalajia kuanza saa mbili na nusu usiku. alisema Scholastica.

Kundi la Makhirikhiri, linaongozwa na Moses Mapela, maarufu kwa jina la ‘Shumba Ratshega’, na kujizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi ya Botswana, ikiwamo nje ya Bara la Afrika.

Pia upendelea kuvaa mavazi ya asili ya ngozi ya Simba, kama katika albam yao ya Makhirikhiri ilikatika kiwango cha juu.

Mbali na shoo hiyo itakayo fanyika JUNE 4 Diamond Jubilee, Juni 6 watajimwaga kwa kufanya mavitu yao kwenye Uwanja wa Uhuru,kisha Juni 12, mwaka huu watamalizia ziara yao kwa kutoa burudani jijini Mbeya.

Baadhi ya wasanii hao kuwa ni ‘Shumba Ratshega’ mwenyewe, Philip Simon, Linda Mosimanagare, Olebile Edson, Nametso Sebele na Motheo Johnson.

Ambapo wapo nchini kwa udhamini wa kituo cha radio cha 100.5 Times FM kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo, Global Publishers, Giraffe View Hotel, Aurora na Tai Five Hotel ya Mwanza.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment