Bunge na wadau katika Maonyesho ya historia yake jijini Mwanza!!

Kundi la watoto washule wakigombea kofia za Karatasi zenye Nembo ya Bunge toka kwa Afisa wa Bunge bi Lily Mraba mara walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi yaliyoanza leo Mjini Mwanza. Maonyesho haya yanatarajia kumalizika tarehe 23 Juni, 2010, ambapo zaidi ya taasisi 100 za Umma zinashiriki. Picha na Owen Mwandumbya

Mtoto ambaye hakufahamika mara moja jina lake, akisoma kwa umakini kipeperushi chenye maelezo kuhusu Historia ya Bunge mara alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi yaliyoanza leo Mjini Mwanza.Kulia ni Afisa wa Bunge, Bi Lina kitosi akimwangalia kwa Makini. Maonyesho haya yanatarajia kumalizika tarehe 23 Juni, 2010, ambapo zaidi ya taasisi 100 za Umma zinashiriki.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment