SAID MACHENJE NDIYE MSHINDI WA DAR SLAM POETRY CHAMPIONSHIP 2010!!

Mkurugezi wa kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance Francaise Didier Martin kushoto akimkabidhi zawadi na kadi mshindi wa shindano la Dar Slam Poetry Championship 2010 Said Machenje kutoka kundi la sanaa la Pambazuko lililoko Mbagala Charambe mara baada ya kuwagalagaza wenzake 24 katika shindano hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam jana
Shindano hilo liliandaliwa na Mrisho Mpoto Production Inc Limited chini ya mrisho Mpoto mwenyewe mshindi wa shindano hilo atawakilisha nchi kwenye shindano la ushairi litakalofanyika katika visiwa vya Reunion na kisha baadae atawakilisha nchini kwenye shindano kubwa litakalofanyika nchini Ufaransa, katika safari yake hiyo ubalozi wa Ufarasa utamghalimia mshindi huyo gharama zake zote za safari atakapokuwa huko mpaka atakapomaliza mashindano.
Lakini pia wadshindi wengine wanne watajifunza kifarasa na kijerumani bure mpaka watakapojua, katika shindano hilo Thabit Muharami alishika nafdasi ya pili wakati Mohamed Gota wa kundi la Pambazuko pia alichukua nafasi ya tatu.
Washindi watatu waliopatikana katika shindano hilo wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa washindi na kuwakabidhi zawadi zao shindano hilo la Dar Slam Poetry Championship lilikuwa limedhaminiwa na Goethe Institute na Alliance Francaise.
Hawa ni vijana kutoka kundi la sanaa za kuigiza la Pambazuko kutoka mbagala Kibirugwa wakishuhudia wenzapoi walipokuwa wakighani kwenye mashindano hayo.
Watu mbalimbali waliojitokeza katika viwanja vya Leaders jijini Dar jana ili kushuhudia mashindano ya Ushariri yaliyoshirikisha vijana mbalimbali wa jiji la Dar es salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment