POPULAR SPORTS BONANZA KUFANYA MAMBO TCC CHANG'OMBE JUNI, 6,2010.

Mkurugenzi wa Popular Sports Bonanza Othman Kazi kulia akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya Movenpick wakati wa mkutano uliohusu bonanza la kuhamasisha mashabiki wa soka ili kufuatilia michuano ya kombe la dunia mara itakapoanza rasmi hapo juni 15.
Kazi amesema bonanza hilo litakalofanyika Juni 6 2010 kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe litashirikisha timu kutoka taasisi mbalimbali na timu hizo zitakuwa na majina ya timu zinazoshiriki kwenye kombe la dunia kama uwakilishi na uhamasishaji wa mashabiki wa soka.
Amezitaja timu hizo kuwa ni Vodacom Tanzania, T. Scan, The Bankers inayoshirikisha benki mbalimbali jijini Dar es salaam, Movenpick, Cocacola, PSI, Zain, Tmes Fm. Nevada Real Estate Fitness na nyingine nyingi, wengine wanaofuatia kwenye picha ni carol rath Afisa kutoka ubalozi wa Afrika Kusini, Msemaji wa Bonanza hilo Cliford Ndimbo, Meneja wa Mpango wa kupambana na Ukimwi PSI Dr. Alex Ngaiza na Mkuu wa Burudani wa bonanza hilo Addull Kipenga.
Othmani Kazi Mkurugenzi wa Popular Sports Bonanza akionyesha zawadi za vikombe zitakazotolewa kwa washindi katika bonanza hilo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment