MISS CHANG'OMBE 2010 KUMEKUCHA, WAREMBO WAJIFUA VIKALI!!

Warembo wanaoshiriki shinfdano la Miss Chang'ombe 2010 wakiwa katika picha ya pamoja kwenye klabu ya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam jana jioni.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Juni 4 wiki hii katika ukumbi huohuo ambapo jumla ya warembo 19 watapanda jukwaani kuwania taji hilo huku burudani ikitolewa na bendi maarufu ya FM Academia ya jijini Dar es salaam pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Machozi.
Aliyewahi kuwa Miss Temeke Jokate Mwegelo akizungumza na warembo hao mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yao jana jioni ambapo pia kamati ya Miss Tanzania ilitembelea kambi ya mazoezi hayo.
Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Miss Chang'ombe wakiwa katika mazoezi jana jioni kwenye klabu TCC Sigara Chang'ombe.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment