KATIBU MKUU HABARI NA UTAMADUNI AKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI!!

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Mh. Seith Kamuhanda akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa DICC uliopo PPF Tower jijini Dar es salaam kwenye mkutano wenye lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo pamoja na kupeana changamoto na mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufuata maadili katika fani nzima ya uandishi wa habari.
Pamoja na mambo mengine ametoa changamoto kwa wahariri wawe chachu katika kuleta mabadiliko na kuhakikisha kuwa habari zinazotolewa zilenge katika kuchochea maendeleo nchini.
(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO).
Wahariri wa Vyombo malimbali vya habari wakiwa wakimsikiliza katibu mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo inayofanyika leo kwenye ukumbi wa DICC jijini Dart es salaam.
Mkurugezni wa Idara ya Habari Maelezo Clement Mshana akiwa katika semina hiyo inayoendelea kwenye ukumbi wa DICC PPF Tower leo.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment