Kumekucha Clouds Tv,kaa tayari kuanzia kesho!

Burudani ni Jadi yao na inazidi kuendelea.! Wana wa Clouds Media Group kupitia Clouds TV wanakuletea burudani ya pekee ya Soka la Ulimwengu,katika levo ya juu kabisa,Mchakato huo wa kuwaletea mpango mzima wa Kandanda unaanza rasmi hapo kesho,yaani Juni 1 kupitia Luninga yao ya Clouds Tv,kila siku saa 3:30 usiku.Watakuwa wanakuletea uchambuzi wa kina ukiambatana na matukio halisi kwenye picha za ubora wa hali ya juu kabisa.Wakiwa katika kipindi chao kiitwacho The road to South Africa 2010 kitakuwa kikichambuliwa na Watangazaji mahiri na wenye vipaji akiwemo Paul James (PJ) pamoja na Shaffih Dauda (Mzee wa number 10). Pichani ni Watangazaji Paul James pamoja na Shaffih Dauda wakiwa ndani ya Studio za Clouds TV tayari kwa kuwaletea mambo mazuri ya kiburudani katika anga ya kisoka zaidi. Picha kwa hsani ya www.michuzijunior.blogspot.com.

Hongera Mkurugenzi Joseph Kusaga kwa kazi nzuri manake Studio inatisha.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment