Uongozi wa timu ya Simba ya jijini umekanusha habari zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa wagombea Hassan Dalali na Hanspope wametolewa katika kinyang'anyiro cha uenyekiti katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni katika klabu hiyo.
Akizungumzia hilo msemaji wa klabu hiyo amesema badala yake kamati inayosimamia uchaguzi inatarajiwa kutangaza majina yatakayoochujwa leo na kutangazwa rasmi hivyo habari zilizojitokeza leo katika baadhi ya magazeti si za kweli.
Habari katika vyombo vya habari zilielezea kuwa wagombea wawili hao katika nafasi ya mwenyekiti Hassan Dalali na Hanspope wameenguliwa kutokana na kutokidhi vigezo katika uchaguzi huo
Katika uchaguzi huo wagombea mbalimbali wamejitokeza ili kugombea nafasi hiyo ya mwenyekiti wa Simba, na waliojitokeza ni Richard Wambura, Aden Rage Hassan Hasanoo, Hassan Dalali pamoja na mmoja wa vigogo wa Friends of Simba na Hanspope






0 comments:
Post a Comment