HASAN DALALI NA ZAKARIA HANS POPE WANAENDELEA NA MCHAKATO WA KUGOMBEA UENYEKITI SIMBA!!


Kamati inayosimamia uchaguzi wa klabu ya Simba leo umepitisha majina yote ya wagombea wa uenyekiti katika klabu hiyo baada ya wagombea hao kuambatanisha nyaraka zote zilizokuwa zikihitajika ili kukidhi vigezo vya kugombea uongozi wa klabu hiyo, tofauti na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti leo, uchaguzi wa viongozi wa Simba unatarajiwa kufanyika Mei 9/ 2010 jijini Dar es salaam.
Afisa habari wa klabu hiyo Cliford Ndimbo amesema leo tarehe 13 mpaka tarehe 18 aprili ndiyo kimetolewa kipindi cha kuweka pingamizi kwa wagombea, kama kuna mwanachama yeyote au mgombea anaona anazo sababu za msingi za kuweka pingamizi kwa mgombea fulani muda ni huu anaweza kuleta pinagamizi lake mbele ya kamati ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa tarehe 19 mei kamati itakaa na kupitia pingamizi kama zitakuwepo na baada ya kupitia pingamizi hizo na kuridhiswa na sababu zilizotolewa katika pingamizi hizo kamati hiyo itapitisha majina ya wagombea tayari kwa kupiga kampeni ili kujiandaa na uchaguzi utakaofanyika mei 9.

Katika uchaguzi huo wagombea mbalimbali wamejitokeza ili kugombea nafasi za mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati mbalimbali nafasi ya mwenyekiti wanaowania ni Richard Wambura, Aden Rage, Hassan Hasanoo, Hassan Dalali pamoja na mmoja wa vigogo wa Friends of Simba na Zakaria Hans pope

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment