Wahudumu wa misaada watekwa nyara Congo!!


Maafisa wanane wa shirika la msalaba mwekundu wametekwa nyara katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wahudumu hao, saba wakiwa ni wenyeji na mmoja Mswizi walitekwa nyara wiki jana walipokuwa wakiendelea na shughuli zao za kutoa misaada kwa wakimbizi walioko mkoa wa Kivu Kusini
Duru zinasema walikamatwa na wanachama wa kundi la Mai Mai Yakutumba karibu na mji wa Fizi. Eneo hilo linafahamika kwa ukosefu wa usalama, na shirika la Red Cross ni mojawapo tu ya masharika machache ya misaada ambayo yamekuwa yakitoa msaada wa chakula na maji safi kwa maelfu ya wakimbizi.
Inaaminika wanamgambo hao waliwashika kwa nguvu wafanyakazi hao na kuwasafirisha mbali zaidi ya mkoa wa Kasakwa.
Hata hivyo msemaji wa shirika hilo mjini Geneva, amekataa kuthibitisha iwapo shirika hilo limeweza kuwasiliana na waasi hao, ingawa inaaminika mazungumzo ya kuwashawishi kuwaachilia mateka wao yanaendelea, serikali ya Uswizi ikisema imeweza kuwasiliana na serikali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment