Mwanasiasa mzungu wa Afrika kusini Eugene Terreblanche ambaye aliuawa na wafanyakazi kwenye shamba lake atazikwa Ijumaa kwenye mji wa Ventersdorp.
Wafanyakazi wawili wameshtakiwa kwa mauaji hayo.
Polisi kadha wamepelekwa katika mji wa Ventersdorp kudhibiti hali ya usalama.
Kuna uwezekano wa kuzuka kwa makabiliano baina ya wafuasi wa bwana Terreblanche na raia weusi.
Eugene Terreblanche anakumbukwa na wengi kwa hisia zake za ubaguzi wa rangi na hata kupinga harakati za kudumisha demokrasia Afrika Kusini.
Serikali ya Afrika Kusini imetupilia mbali madai kwamba mauaji ya Terreblance yalichochewa na chuki dhidi ya wazungu.
Makundi ya wazungu na vyama vya upinzani vinamlaumu kiongozi wa tawi la vijana la ANC Julius Malema kwa kueneza nyimbo zenye matamshi makali na ambazo zilivuma nyakati za kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Mfano wa nyimbo hizo ni ule unaowahimiza weusi "kumpiga risasi mkulima".
Hata hivyo chama cha ANC kimekanusha madai ingawa kilikiri kwamba wimbo huo ulichochea utengano.
Wimbo huo umepigwa marufuku.

0 comments:
Post a Comment