Waziri Mkulo alipotembelea bahari beach Hotel!!

Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (kulia) akimwonyesha kitu jana jioni jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bahari Beach Hotel Abdalah Hiblo( kushoto) . Waziri huyo alikwenda Hotelini hapo kwa niaba ya Rais Kikwete ili kujionea hatua za ukarabati zilizokwishafikiwa mara baada ya Hoteli hiyo kubinafishwa kwa Mwekezaji kutoka Libya.
Hapa akipita katika maeneo mbalimbali ya hoteli hiyo na kujionea maendeleo ya ukarabati wa hoteli hiyo
Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (katikati) akisisitiza jambo jana jioni jijini Dar es salaam kwa viongozi wa Hoteli ya Bahari Beach ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni mara baada ya kukamilika ukarabati wake.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Hotel hiyo Gerald Schravan(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji Abdalah Hiblo(kulia).

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment