Mlinda mlango wa Liverpool Pepe Reina amesaini mkataba mpya wa miaka sita na klabu yake ya Liverpool hatua itakayomuweka Anfield hadi mwaka 2016.
Reina, mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na Liverpool mwaka 2005 akitokea Villarreal na ameshadakia timu hiyo michezo 250.
Mlinda mlango huyo raia wa Hispania ameeleza kupitia mtandao wa Liverpool:"Nina furaha isiyo kifani, huenda ni taarifa njema kwa maisha yangu kwamba nitakuwa hapa kwa miaka sita ijayo."
Reina ameongeza kueleza: "Mke wangu aliniambia tangu mwanzo anapenda kuishi hapa."
Pia wachezaji wengine muhimu wa klabu hiyo waliokwishamwaga wino hivi karibuni kwa mkataba wa muda mrefu ni pamoja na Fernando Torres, nahodha Steven Gerrard, Dirk Kuyt, Daniel Agger na Yossi Benayoun.

0 comments:
Post a Comment