Jeshi la Marekani lasitisha safari kutoka Kyrgyzstan!!


Jeshi la Marekani limesitisha safari zote za ndege za vikosi vyake kutoka Kyrgyzstan kuelekea Afghanistan, kutokana na hali ya wasiwasi inayojiri Kyrgyzstan, baada ya kuzuka kwa harakati za upinzani dhidi ya rais wa nchi hiyo.
Hatua hiyo ya usitishaji wa safari za ndege za wanajeshi kutoka kituo cha wana-anga cha Manas, ambayo haijulikani itadumu kwa muda gani ilifikiwa na makamanda wa jeshi la Marekani nchini Kyrgyzstan.
Msemaji wa jeshi la Marekani hakutoa ufafanuzi zaidi kuhusu uamuzi huo.
Alisema alisema safari hizo zitaanzishwa tena punde baada ya hali ya usalama nchini Kyrgyzstan kuwaruhusu kufanya hivyo.
Kituo cha wana-anga cha Manas ni kituo muhimu cha uchukuzi kwa operesheni za kijeshi zinazo-ongozwa na Marekani dhidi ya kundi la Taliban nchini Afghanistan.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment