Watu 7 Kenya wafariki kwa ulevi!!


Watu saba wamefariki baada ya kunywa kinywaji cha kulevya, maarufu kama chang'aa, katika mtaa wa Shauri Moyo, mjini Nairobi, na wengine wawili wako katika hali mahututi.
Maafisa wa polisi waliweza kufika mahali hapo na kuwasaidia watu walioathirika.
Inaarifiwa kwamba watu wengine pia walipoteza uwezo wa kuona, baada ya kunywa kinywaji hicho, na baadhi yao kufikishwa katika hospitali kuu ya Kenyatta, huku wengine wakipata matibabu katika mtaa huohuo.
Hata hivyo maafisa wa polisi hawajaweza kuthibitisha kama kuna yeyote aliyekamatwa kwa kutayarisha kinywaji hicho.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment