WATEJA WA ZANTEL ZANZIBAR KUNUFAIKA NA PROMOSHENI YA CHOMOKA NA VESPA!

Zantel leo imezindua promosheni ya CHOMOKA NA VESPA maalum kwa wakazi wa Zanzibar. Promosheni hii itawawezesha wateja wa zantel kisiwani humu kupata nafasi ya kujishindia pikipiki aina ya Vespa ambayo ni chombo maarufu sana cha usafiiri visiwani humo..
Akizungumwa na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Meneja masoko wa kampuni ya Zantel Bw. William Mpinga alisema kwamba zawadi katika promosheni hiyo ni pamoja na Vespa 8, Baiskeli za kisasa 24, Simu zinazotumia umeme wa jua 24 pamoja na vocha 40 za muda wa maongezi wa Tsh 10,000.

“Tutakuwa tukitoa Vespa 1 kila wiki, baiskeli za kisasa 3, simu za mkononi zinazotumia mwanga wa jua 3 na vocha 5 za muda wa maongezi wa Tsh 10,000 kila wiki kwa muda wa wiki 8 kwa watakaobahatika kujishindia zawadi hizi” alisema Bw. William.
Meneja huyo ameendelea kusema kwamba Zantel imeamua kuzindua promosheni hiyo ili kuwazawadia wateja wake wa Zanzibar ambao wamekuwa wateja wa muda mrefu wa kampuni hiyo na kwamba zawadi hizo ni chaguo la wateja wa visiwani hapo kwani ni vitu ambavyo vinatumika na wakazi hao katika maisha yao ya kila siku.

Ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja wa zantel atatakiwa kuweka muda wa maongezi wa Tsh 1,000 au zaidi na kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno VESPA kwenda namba 15583. Ujumbe huo utatozwa Tsh 350 pamoja na VAT. Mteja anaweza kutuma SMS nyingi kadri awezavyo ili kujiongezea nafasi za kushinda.

Droo za promosheni hii zitafanyika kila Jumatatu ambapo washindi watapigiwa simu na kutaariwa kuhusu ushindi wao na hatimaye kupewa zawadi zao.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment