Wanajeshi waimarisha Doria Nigeria!!

Wanajeshi wa Nigeria wanaendelea kushika doria katika vijiji kadhaa viungani mwa mji wa Jos, kufuatia mauaji ya mamia ya watu, kwenye mapigano ya kikabila.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo amesema wanajeshi hao wanatumia magari ya kivita, ili kuhakikisha ghasia kama zile za siku ya jumapili hazitokei tena. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bii Hillary Clinton, ameelezea wasi wasi wa serikali yake, kufuatia mauaji hayo. Bii Clinton ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliohusika na mauaji hayo.
Hapo jana waliouawa, wengi wao wakiwa kina mama na watoto walizikwa kwenye makaburi ya pamoja.
Wakati huo huo kaimu rais wa Nchi hiyo, Goodluck Jonathan, amemfuta kazi mshauri mkuu wa serikali wa masuala ya ulinzi wa taifa. Jeshi la nchi hiyo ilitangaza amri ya kutotoka nje mjini humo tangu Januari mwaka huu, kufuatia mauaji ya zaidi ya watu mia mbili kwenye mapigano kati ya Wakristo na Waislamu

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment