Meneja wa Liverpool Rafael Benitez amewalaumu wachezaji wake baada ya kufungwa bao 1-0 na Wigan, kwa kuwaeleza hawana ari ya kushinda.Benitez ameiambia BBC "amekatishwa tamaa."
Ameongeza kusema"Kipindi cha kwanza hatukufanya lolote la maana linalohitajika. Ni vigumu kuelezea.
Amezidi kuiambia BBC, "Wakati wa mapumziko tulielezana kusahihisha pale tulipokosea. Tulifanya makosa mengi sana na tulicheza haraka mno."
Huu ni mchezo wa tisa Liverpool inapoteza kati ya michezo 29 ya Ligi Kuu ya England, hali ianayoiacha ikiwa na kibarua kigumu kuweza kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao.





0 comments:
Post a Comment