KILIMANJARO MUSIC AWARD YAWAFUNDA WANAMUZIKI LEO!!

Wasanii wakijiandikisha kabla ya kuingia kwenye chumba cha semina katika ukumbi wa paradise city hotel jijini dar leo, Semina iliyoandaliwa na waandaaji wa tuzo hiyo Kilimanjaro Tanzania Music Awards ikiwahusisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya na cha kale ili kuwekana sawa namna ya kuteua wanamuziki bora wa mwaka huu watakavyoteuliwa.

Kilimanjaro Music Award hufanyika kila mwaka na kutoa tuzo kwa wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, muziki wa kale, muziki wa Taarab na muziki wa Injili pia, tuzo hii imekuwa ikiwasaidia wanamuziki mbalimbali kujiangalia upya mara zinapokuwa zimefanyika tuzo hizi lili kutathimini kazi zao na kuziboresha zaidi ikiwa ni pamoja na kujianda kwa tuzo zitakazofuatia kama watafanikiwa kuingia kwenye kinayang'anyiri hicho.
Jafaraia na Lady Jay Dee wakizungumza kabla ya kuanza kwa semina hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam.
Master J katikati akiwa na Mwanamuziki AY na mmoja wa wanamuziki waliohudhuria semina hiyo.
Mr Ebbo kulia na Mgosi wa Kaya kutoka kule TangaMkoloni na wanamuziki wengine wakibadilishana mawazo katika semina hiyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment