Wanajeshi wajinufaisha na madini DRC!!

Shirika la kutetea haki za bianadam la Global Witness linasema limepata ushahidi kuwa wanajeshi waliokuwa waasi katika eneo la mashariki mwa Congo wanajinufaisha na biashara ya madini nchini humo.
Waasi hao wa zamani kutoka chama cha CNDP wanasema wameweza kudhibti migodi ya madini kwa kiwango kikubwa kuliko wakati walipokuwa waasi.
Shirikika hilo limeshtumu serikali ya jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo na jamii ya kimataifa kwa kutochukua hatua madhubuti kuwaondoa watu waliojihami katika migodi nchini humo. http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment