SIMBA YATANGAZA UBINGWA WA LIGI KUU BARA, BAADA YA KUIBANJUA AZAM FC 2-0 UWANJA WA UHURU!!

Mashabiki wa timu ya Simba wakifurahia ubingwa wa timu yao.

Timu ya Simba ya jijini Dar es salaa leo imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Vodacom inayoelekea ukingoni baada ya kuitandika Azam FC magoli 2-0 kwenye kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo.
Mpaka Simba inakutana na timu ya Azam FC ilikuwa haijafungwa mchezo hata mmoja katika ligi hiyo ambapo imeshinda michezo 18 na kutoa droo michezo miwili bado haijacheza michezo miwili kati ya Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro na watani wao wa jadi timu ya Yanga pia ya jijini Dar es salaam.
Katika michezo hiyo yote Simba imefanikiwa kujikusanyia pointi 55 mpaka katika mchezo wa leo ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika michezo iliyobaki, ambapo Yanga ndiyo inafuatia kwa mbali kwa kuwa na pointi 45 ambazo hata kama itafanikiwa kushinda michezo yote mitatu iliyobaki itafikisha pointi 54 tofauti ya pointi moja na timu ya Simba ambayo tayari ina pointi 55.
Katika uwanja wa Uhuru leo nyota wa mchezo alikuwa mchezaji wa kulipwa wa timu hiyo mkenya Mike Barasa ambaye aliweza kuifungia magoli mawili timu ya Simba katika kipindi cha Kwanza na cha pili cha mchezo huo, matokeo hayo yamedhihirisha ubaora wa kikosi cha timu ya Simba kinachonolewa na mzambia Patrick Phiri kwani toka ligi hiyo ianze timu hiyo haijapoteza mchezo hata mmoja
Timu ya FULLSHANGWE inawapa hongera wanasimba wote popote walipo kwa ushindi wao huo na kujitangazia rasmi ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2010/2011 hongereni sana wachezaji wa simba mmefanya kazi kubwa na mlistahili kupata mlichokipata leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment