AISHA MADINDA AREJEA TWANGA NA KUKAMUA VILIVYO MANGO!!

Bendi wa African Stars wana Twanga Pepeta, leo inatoa ofa ya wanawake kuingia bure katika shoo yake ya TCC Club, Chang'ombe leo ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Wanawake Duniani. Kwa mujibu wa kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu, wanawake watakaohudhuria onesho hilo kuanzia saa moja hadi saa nne usiku wataingia BURE na watakaofika baada ya muda huo wataingia kwa kiingilio cha kawaida.
Pia kwa wale ambao hawafahamu ujio wa Aisha Mbegu 'Madinda', wanajulishwa kuwa mwanadada huyo aliyeko kushoto katika picha amerejea jukwaani tena kwa kishindo na usiku wa kumkia leo alikuwa pale Mango Garden akifanya vitu vyake kama kawa, kama unavyomuona akiwajibika vyakutosha mdau

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Aisha tulia dada,
    wewe mkali na una fans wengi.
    kaza buti,


    disminder.

Post a Comment