NANI KAMA SIMBA JAMANI, YAIKUNG'UTA AZAM FC 2-0 NA KUTWAA UBINGWA WA 2010/2011!!

Wachezaji wa timu ya Simba wakimbeba juujuu kocha wa timu hioyo mzambia Patrick Phiri mara baada ya kumalizika kwa mpambano kati ya timu hiyo na Azam FC uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru na kuitangazia ubingwa timu ya Simba baada ya kuipiga kumbo timu ya Azam Fc na kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika michezo iliyobaki, hivyo Simba inatawazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2010/2011.
Mashabiki wa timu ya Sim,ba wakishangilia huku wakiwa wamebeba sanamu ya myama Simba mara baada ya timu yao kuchukua ubingwa leo kwenye uwanja wa Uhuru baada ya timu hiyo kuifunga timu ya Azam FC na kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika michezo iliyobaki.

Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya mchezaji wa timu hiyo Mike Barasa kufunga goli la kwanza.


Mmoja wa mashabiki wa timu ya Simba akicheza huku akiwa nekedi katika kushangilia ushindi wa timu yake kaaaazi kwalikweli.

Wachezaji wa Simba wakishangilia huku wakiwa wameshika bango lenye maandishi ya kuipongeza timu hiyo.


Mashabiki wa kiongea na mmoja wa wanachama wa Frieds of Simba mara baada ya timu hiyo kuchukua ubingwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru


Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa shamrashamra kwabwa kwenye uwanja wa Uhuru

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment