SIMBA KUKIPIGA NA ZANZIBAR OCEAN VIEW KESHO!!

Timu ya Simba inatarajiwa kukipiga na timu ya Zanzibar Ocean View katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa hapo kesho jumanne kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam msemaji wa timu ya Simba Cliford Ndimbo amesema mchezo huo ni wa kujipima nguvu na kurekebisha makosa kadhaa katika kikosi hicho ili kuiweka sawa kwa michezo inayokuja.
Ndimbo ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni shilingi 1000 mzunguko, jukwaa la kijani itakuwa shilingi 2000, jukwaa la kuu shilingi 3000 na VIP kiingilio kitakuwa 5000 mashabiki wote wa simba wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuona timu yao itakapokwaruzania na Zanzibar Ocean View.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment