Mwigizaji wa filamu za Kitanzania Steven Kanumba ameibuka mwigizaji bora wa mwaka katika shindano lililokuwa likiendeshwa na Redio Clouds lililoshirikisha waigizaji mbalimbali wa kiume imefahamika leo.
Steven Kanumba aliwabwaga wenzake wanne alioingia nao katika tano bora baada ya kupigia kura na wadau mbalimbali kupitia ujumbe wa simu blogu ya Dina Marios na simu zilizokuwa zikipigwa kwenye kipindi cha Leo Tena kinachotangaza na Dina Marios mwenyewe na kurushwa na redio hiyo kila siku kuanzaia saa tatu mpaka saa saba mchana.
Kanumba amewabwaga Hemed, Yusuph Mlela, Cloude na Raymond Kigosi (Ray) matokeo hayo yametanzagwa nza redio hiyo leo yapata saa nne asubuhi na mara baada ya kutangazwa watu mbalimbali wametuma salamu na kupiga simu za kumpongeza mwigizaji huyo kwa kushinda katika kinyang'anyiro hicho, kwa upande wa walioshindwa ni changamoto kwa kurekebisha pale walipokosea ili wakati mwingine waweze kufanya vyema






0 comments:
Post a Comment