Mshambuliaji wa soka wa Nigeria Endurance Idahor amefariki dunia baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mechi nchini Sudan siku ya Jumamosi.Idahor, mwenye umri wa miaka 25, aliyekuwa akiichezea klabu ya Al Merreikh alianguka uwanjani wakati wa mchezo wa ligi na Al Amal mjini Omdurman.
Inaaminika alikufa akiwa njiani akipelekwa hospitali baada ya kugongana na mwenzake katika eneo la penalti.
Kwa mujibu wa afisa mmoja aliyekataa kutajwa jina, amesema ulikuwa ni mgongano wa kawaida.
Aliendelea kueleza,"Alianguka na sasa amekufa. Ni tukio la kustusha kwa wapenda soka wote nchini Sudan."





0 comments:
Post a Comment