KATIBU MKUU WA CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AENDELEA VIZURI!!

Hali ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, imeimarika kiafya baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar leo.

Kuimarika kwa afya ya mwanasiasa huyo mwandamizi wa kambi ya upinzani na Katibu wa CUF imeondoa hofu na minong’ono iliyoenea jijini kwamba Maalim Seif, amefariki dunia.
Maalim Seif amesema tatizo linalomsumbua ni kupanda kwa shinikizo la damu na kwamba juzi lilimsababishia kushindwa kusafiri.
Amesema shinikizo la damu lilipanda ijumaa saa 11 jioni alipokuwa akisubiri kupanda ndege kwenda Oman kwa ajili ya shughuli zake binafsi.
“Kweli nilipata matatizo ya kiafya kidogo ijumaa iliyopita kama kwenye saa 11 jioni wakati nasubiri kwenda Oman kwa shughuli binafsi, ndiyo hali ilipobadilika ghafla... lakini sasa naendelea vizuri tatizo kubwa ni high blood pressure (kupanda kwa shinikizo la damu) ila tangu nilipolazwa haijapanda tena.

“... Ugonjwa huu unanisumbua tangu mwaka 1989 lakini kwa kipindi kirefu ulikuwa under control (chini ya uangalizi) ila kwa sasa naona limekuwa kubwa mno, nadhani ni kwa ajili ya kazi nyingi.
“Madaktari wamenipima moyo wameona upo safi, damu safi na mapigo ya moyo yapo safi sasa wamenipumzisha na Mungu akipenda leo jioni au kesho Inshaalah nitaruhusiwa,” alisema Maalim.
"Kwa sasa hali yangu imeimarika na nipo chini ya uangalizi wa madaktari kwa ajili ya kupumzika wakati wakiendelea kudhibiti shinikizo hilo la damu alisema mkongwe huyo wa siasa visiwani Zanzibar."
Aidha, Maalim Seif liwashukuru Watanzania walioguswa baada ya kupata taarifa za ugonjwa wake na wengi wao kmtumia salamu za pole hali iliyomfariji na kuona jinsi wananchi wanavyoshirikiana.

Waandishi wa habari wa televisheni ya TBC-1 wakimhoji Maalim Seif katika hospitali ya hindu mandal leo.

Maalim Seif Shariff Hamad akipokea mkono wa pole toka kwa Dk. Swedi ambaye ni mmoja wa watu kadhaa waliokwenda kumjulia hali leo hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar es salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment