Serikali yaendelea kufanyia maboresho ya utawala Bora!!


Benjamin SaweMaelezo Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa Bara la Afrika lina uwezo wa kuendeleza malengo ya umajimuni wa Kiafrika (Pan –Africanism) kwa kujikumbusha misingi bora ya kiutawala iliyokuwepo tangu zama za mababu kabla ya wakoloni.Waziri Membe aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Francis Malambugi wakati akifungua semina ya tathmini ya utawala bora nchini iliyoandaliwa na APRMPia alisema baadhi ya jamii zimeweza kutajwa kuwa za kwanza kiustaarabu duniani kutokana na ushirikiano wa pamoja baina ya jamii hizo na Bara la Afrika lililokuwa na misingi adhimu ya kiutawala na kidemokrasia.
Alisema mchakato wa APRM umekuja ili kuipa fursa Afrika kujitazama na kubaini nguvu ilizonazo na udhaifu hivyo kuweka kanuni za kuyatatua matatizo yake kwa kutumia wataalamu wake ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wa maendeleo.Kwa upande wa Serikali Waziri Membe alisema inaendelea kufanya maboresho katika Mhimili wa Mahakama,Sekta ya Utumishi wa Umma,Sekta ya Fedha ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa Sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha katika mchakato wa uchaguziAlisema maboresho mengine ambayo Serikali imeendelea kuyafanya ni ya Sheria ya kuhakikisha kuwa Serikali inagharimia dawa muhimu hasa kwa wagonjwa wa ukimwi pale inapowezekana bila ya kuwatoza fedha ikiwa ni pamoja na kutenganishwa kwa Siasa na Biashara.
Katika semina hiyo ya siku moja ya kitaifa iliyohusu kuhakiki Ripoti ya Nchi kuhusu utawala bora iliyoandaliwa na APRM Balozi Malambugi alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernad Membe.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment