Klabu ya ngumi ya Ashanti kuzinduliwa hivi karibuni!!


KLABU mpya ya Mchezo wa Ngumi ya Ashanti inatarajiwa kutambulishwa kwa klabu zingine za mchezo huo Ijumaa katika ukumbi wa CCM Ilala Boma Dar es Salaam.

Kocha mkuu wa klabu hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema Dar es Salaam leo kuwa klabu hiyo yenye mabondia 9 itatambulishwa kwa klabu zingine ili itambulike kuwa ni miongoni mwa klabu zinazoendeleza mchezo wa ngumi Tanzania.

Alisema utambulisho huo utakuwa chini ya taasisi ya Kinyogoli Foundation inayosimamia kwa karibu mchezo wa ngumi Tanzania kabla ya uzinduzi wake utakaofanyika Machi mwaka huu.

Super D alisema katika hafla hiyo kutakuwa na Klabu za Simba, Vingunguti, Amana, na wenyeji Ashanti ambapo kila klabu itawakilishwa na mabondia watatu.

Amesema klabu hiyo imeanzishwa hivi karibuni na inaundwa na mabondia kama Juma Salum 'Jeshi, Yahaya Hamis, Ramadhani Ngumbo, Ramadhani Kassimu na Abdujerry Kadil

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment